Introduction de AFRIC Africa

AFRIC Africa ni shirika gani?

AFRIC Africa ni shirika lisilofuata faida za kiuchumi (non-profit organization: NPO) . Lilianzishwa Aprili 2004 katika Kyoto, Japani.

AFRIC Africa lilianzishwa na watafiti vijana na wenzao wenye uzoefu wa kufanya utafiti wa kimasomo mijini na vijijini mwa Afrika. Kwa kupitia utafiti wa muda mrefu katika Afrika, wanachama walipata hisia za kutaka kujua zaidi maisha ya wanajamii waishio Afrika. Wakati huo huo, wanachama wamejua umuhimu wa kuunganishia utafiti wa kimasomo na kazi za ushirikiano pamoja na wanajamii waishio Afrika.

AFRIC Africa linatafuta namna za kujengea misingi ya jamii ambazo wanajamii wataweza kuishi na usalaama na furaha. Sisi tutatekeleza kazi hizo kwa kugawana uzoefu wetu unaotokana na utafiti baina ya watu wa Japani na Afrika.

AFRIC Africa linashughulika na nini???

AFRIC Africa linatekeleza kazi za ushirikiano na utafiti katika nchi mbalimbali za Afrika. Wakati huo huo, tunapenda kuwatolea Wajapani furusa za kujua/kuelewa zaidi kuhusu matukio na mambo mbalimbali za Kiafrika.

1. Tunashirikiana na wanajamii wa Afrika katika kazi za kujengea jamii ambazo watu wanajitegemea/wanatosheka kuishi chini ya miongozo yao yenyewe.
k.m. Tunashirikiana na NGOs (Shirika lisilo la kiserikali) za Tanzania. Tunatamani ushirikiano wetu kwa hizo NGOs uwatilie wanajamii mioyo zaidi ya kuboreshea jamii na mazingira zao.

2. Tunashughulikia kazi za kuwasaidia wanajamii waishio Japani kujua/kuelewa zaidi matukio na mambo mbalimbali za Kiafrika.
k.m. Wanachama wanatembelea kwa shule, ofisi na taasisi mbalimbali katika Japani na wanasimulia na wanaeleza mambo yanayohusika na Afrika. Kwa kupitia kazi kama hizi, tunawapa Wajapani furusa ya kujua habari za Kiafrika ambazo kawaida hazipatikani kwa urahisi kwa kupitia vyombo vya habari katika Japani.

3. Tunashughulikia kazi za kuleta maelewano na mabadilishano mazuri ya mawazo baina ya watu waishio katika Japani na Afrika.
k.m. Wanachama wetu wanatembelea shuleni kwa nchi za Afrika. Wanasimulia habari kuhusu Japani na wanapokea maswali yanayohusu Japani na wanatoa majibu hapo hapo.

Ukitaka habari zaidi, tuandikie barua pepe: info(at)afric-africa.org
Tunakaribisha kuwasiliana nasi kwa Kiswahili. Hamna shida !